TEMBELEA HII WEBSITE

EMAIL YANGU NI!!!!!!

Thursday, October 23, 2014

NGOMA DRAW YANGA 0-0

Yanga imetoka sare ya bila kufungana katika mechi yake ya 

kirafiki dhidi ya CDA mjini Dodoma, leo.

Mechi hiyo imepigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma 

na kumalizika bila bao huku mechi ikiwa na ushindani utafikiri ya 

ligi kuu.

Yanga iko njiani kwenda Shinyanga kupambana na Stand United 

katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto amesema wataondoka kesho 

asubuhi kwenda Shinyanga tayari kabisa kwa mechi yao dhidi ya 

wenyeji wao stand..




Sunday, July 20, 2014

TAIFA STARS 2-MOZAMBIQ 2

MPIRA UMEKWISHA:

Dk 87 Isaac Calvaho anapokea pasi ya Domingues baada ya Yondani kupigwa kanzu na kufunga kiulahisi kabisa
Dk 86, shuti la Ulimwengu linagonga mwamba na Msumbiji wanauchukua mpira na kupeleka shambulizi kali


Dk anatoka Samatta na nafasi yake inachukuliwa na Simon MSuva
Dk 76, Stars wanamtoa Bocco anaingia Haruna Chanongo.
GOOOOOOO Dk 71 Mcha anafunga penalti ya kiufundi kabisa....Stars mbili

PENATIII Dk 70, Samatta anaangushwa na mwamuzi anatoa penalti
Dk 69, shuti kali la Samatta linapaa juu ilikuwa ni baada ya kupokea pasi ya Kapombe

Dk 68, Domingues anapiga shuti kali nje 
Dk 66, Stars wanafanya shambulizi tena lakini mpira wa Ulimwengu unawahiwa kabla ya kumfikia Bocco.

GOOOOOOO Dk 65, Mcha anaifungia Stars bonge la bao baada ya kuunganisha krosi ya Nyoni.

Dk 58, yeye na lango lakini beki anawahi na kuokoa
Dk 57, Stars wanamtoa Ngassa anaingia Hamis Mcha  'Vialli'

Dk 54, Stars wanafanya shambulizi na shuti la Bocco linaokolewa na kipa wa Msumbiji


Dk 53 Samatta anafunga lakini ni offside
GOOOOOOO Dk 47 anamchambua kipa Dida na kufunga bao...MSUMBIJI WANAPATA BAO

DK 46 Yondani anafanya faulo inakuwa penalti.
MAPUMZIKO:
Dk 41, Khan anamuangusha Samatta, analambwa kadi ya njano lakini faulo aliyopiga Joshua ni butu.
Dk 37 Cannavaro anakosea lakini Pelembe anapiga shuti dhaifu

Dk 31, Samatta anawatoka mabeki wa Msumbuji na kupiga shuti kali, lakini beki anaweka kichwa na inakuwa kona. Ngassa anapiga kona na Bocco anapiga kichwa, kipa anadaka kilahisi

Dk 25, Cannavaro anapiga kichwa safi, lakini kipa wa Msumbiji anafanya kazi ya ziada kuokoa.

Dk 20, Elias Pelembe wa Msumbuji anapiga shuti kali lakini linapita nje..Msumbuji wanashambulia zaidi

Dk 14, Domingues wa Msumbiji anaingia na kupiga shuti lakini anashindwa kulenga.


dk 8 Msumbiji wanafanya shambulizi kali, lakini Cannavaro anaokoa.
Dk 5, Nyoni anapiga shuti kali baada ya kupokea pasi ya Ngassa, lakini kipa anadaka kwa ulaiini.
Dk 4, Cannavaro anapiga mpira akiwa amebaki na lango, lakini unapaa.
Dk 1&3 hakuna shambulizi kwenye lango lolote.



http://ramadhani-abubakari.blogspot.com